Test Your Bible Knowledge.
Across
- 3. Ni kipimo gani katika nyakati za kale kilicholingana na homeri na bathi kumi? (Luka 16:7)
- 4. Mshahara wa dhambi ni nini? (Waroma 6:23)
- 6. Ni Mwisraeli gani mashuhuri aliyekuwa na wana “wasiofaa kitu”? (1 Samweli 2:12)
- 7. Ni nani aliyeitwa “mama ya kila mtu anayeishi”? (Mwanzo 3:20)
- 9. Yesu alimpa Simoni mwana wa Yohana jina gani? (Yohana 1:42)
- 10. Wanafunzi wa Yesu walikuwa wakivuta makasia kuelekea jiji gani walipomwona Yesu akitembea juu ya bahari? (Marko 6:45-49)
- 12. Nyuzi ndefu katika chombo cha kufumia huitwaje? (Isaya 38:12)
- 14. Mtu yeyote anayetaka kuwa wa kwanza kati ya ndugu zake anapaswa kuwa nani wao? (Marko 10:44)
- 16. Ni mwana yupi wa Noa aliyefanya jambo lililosababisha mwana wake, Kanaani, alaaniwe? (Mwanzo 9:22-25)
- 18. Yehova alimwagiza Abramu aondoke jiji gani la Wakaldayo? (Mwanzo 11:31; 12:1)
- 19. Ni eneo la kabila gani ambalo baadaye liliwakilisha eneo la kaskazini kabisa mwa nchi ya Israeli? (Waamuzi 20:1)
- 21. Ni ofisa gani Mroma wa Yudea aliyemwacha Paulo akiwa amefungwa kwa sababu ya kutaka kupata kibali cha Wayahudi? (Matendo 24:27)
- 22. Daudi alikubali kupewa adhabu gani kati ya zile adhabu tatu alizowekewa kwa kukosa kumtii Mungu na kuwahesabu Waisraeli? (2 Samweli 24:12-15)
Down
- 1. Ili kuonyesha ukuu wa Yehova, Isaya alisema kwamba Yehova anaweza kupima “maji” katika nini Wake? (Isaya 40:12)
- 2. Makao ya Adamu na Hawa yaliitwaje? (Mwanzo 2:15)
- 4. Gavana Feliksi alihakikisha kwamba Paulo ametoka katika jimbo gani? (Matendo 23:34)
- 5. Mama ya Sulemani alimfumia nini siku yake ya arusi? (Wimbo wa Sulemani 3:11)130 Y
- 8. Ni vazi gani lililofanana na aproni ambalo kuhani mkuu alivaa juu ya koti lake la buluu lisilo na mikono? (Kutoka 28:4, 31)
- 11. Ni nani aliyekuwa mkuu wa jeshi la Absalomu, wakati Absalomu alipoasi dhidi ya Daudi, kisha akawa mkuu wa jeshi la Daudi baada ya Absalomu kuuawa? (2 Samweli 17:25; 19:13)
- 13. Malaika aliyemweleza Maria kwamba alikuwa amechaguliwa kumzaa Yesu, aliitwa nani? (Luka 1:26-31)
- 15. Katika siku za Sulemani, ni kundi gani la meli lililobeba fedha, pembe za tembo, sokwe, na tausi hadi Israeli? Meli za______(1 Wafalme 10:22)
- 17. Ni jiji gani lililokuwa la pili kutekwa na Waisraeli walipovamia Kanaani? (Yoshua 8:18, 19)
- 20. Yule mtu aliyepooza ambaye aliponywa na Petro aliyekuwa amelala juu ya kitanda chake kwa miaka minane aliitwaje? (Matendo 9:33, 34)